top of page
A7R02202-2_edited.jpg
projects.

Kuhusu

Sauti Ya Bwana ni nini?

 

Sauti Ya Bwana ipo iliweze kutoa tumaini kwa wale wanaotafuta amani ya moyo, njia bora ya kuishi maisha yao ya kila siku, na majibu kwa mizigo mizito wanayobeba kila siku, katika dunia ambayo mara nyingi haina mwangaza wa kiroho…tunashiriki tumaini. Sauti Ya Bwana inazalishwa kwa Kiswahili, mojawapo ya vipindi vya lugha kumi vya Christians Broadcasting Hope (CBH).

Kwa Nini Tumaini?

 

Tumaini ndilo hutupa nguvu za kuamka kila asubuhi. Tunatumaini kwa siku njema, tunatumaini kwa maisha bora ya baadaye, tunatumaini kwa njia bora ya kuishi. Masuala haya yote yanayoathiri maisha yetu huzungumziwa katika mijadala yetu. Tumaini pia lina uhusiano na imani na upendo. Kupitia vipindi vyetu, tunajitahidi kuleta tumaini la kweli. Ni tumaini linalopatikana vyema zaidi katika kumjua Yesu, Mungu aliye hai.

A7R02420.jpg

Sauti Ya Bwana Mtayarishaji

 

Obed Okech Olenja ni mhudumu aliyewekwa wakfu na Kanisa la Mungu katika Afrika Mashariki, Kenya. Yeye ni Mkenya kwa uraia, Kaunti ya Vihiga. Yeye ni mwalimu katika Chuo cha Mafunzo cha Kimataifa cha Trelliss. Ana shauku ya kuufikia ulimwengu na ujumbe wa Yesu Kristo, haswa watu wa Afrika. Kwa kuwa anajua Kiingereza na Kiswahili, watu wengi wanaozungumza Kiswahili wataweza kunufaika na vipindi vya Christian Broadcasting Hope (CBH).

​

Obed ana Shahada ya Uzamivu ya Theolojia, shahada ya uzamili katika mawasiliano (Media Studies), Stashahada ya Juu ya Saikolojia na Ushauri, ambayo imempa uwezo wa kujitolea katika huduma ya Yesu Kristo. Kama mtayarishaji na meneja wa Christian Broadcasting Hope, Swahili nchini Kenya, amedhamiria kuwakaribisha viongozi na wachungaji wa Kanisa la Mungu, kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu litakalotoa changamoto na kukidhi mahitaji ya watu, wanaohitaji tumaini.

A7R02229-Pano-3.jpg

"Nimekuja ili muwe na uzima, tena muwe nao tele." — Yesu

about.

Sikiliza

A7R02284-3.jpg
contact.

Mawasiliano

Asante kwa kutuma!

bottom of page